DIBAJI
Usuli wa kihistoria ya jamii ya mijikenda
Kabla ya historia ya historia kuchorwa kama mbinu ya uhifadhi katika kumbukumbu za wakati, kulikuwa na ulimwengu ambao roho za binadamu zilicheza na kuwiana na tenzi na sauti ya ulimwengu na kukawa na maelewano. Hii ilikuwa kawaida ya desturi ya jamii ya Mijikenda, waliokua na makao yao kando ya pwani ya mashariki ya Afrika, mahali ambapo mwangwi wa zamani ulinong'oneza kupitia misitu minene ya ‘Kaya’ iliopewa sifa za kuwa na vipawa na kufahamika kama makaazi ya mababu waliotangulia na basi kuwa mahali takatifu.Hapa, katika utoto huu wa ustaarabu, Wamijikenda walistawi chini ya dari ya anga za ikweta, maisha yao ya kuhisishwa na mchanganyiko wa mila, kiroho, na uadilifu wa jamii.
Utawala wa Mijikenda ulionyesha muundo wao wa kisasa wa kijamii. Iliongozwa na baraza la wazee na machifu, ambao waliwaongoza watu wao kwa hekima na maono ya kujijenga kam jamii. Uchumi wao ulistawi kupitia kilimo, uwindaji, na biashara, na masoko yao yalikuwa ni biashara ya kubadilishana utamaduni.
Moyo wa imani yao ulijaa heshima kubwa kwa ‘Mulungu’ Mungu mkuu, na heshima kwa mababu, ambao roho zao zililinda jamii zao.
Maingiliano ya Ulaya na Afrika kutoka karne ya 15
Walakini, utulivu wa jamii hii ulipangwa kuvurugwa na meli za kigeni zilizoa toa nanga msimu wa upeo wa macho. Kuwasili kwa mpelelezi wa ureno Vasco da Gama mwishoni mwa karne ya 15, kuliashiria mwanzo wa kipindi cha ushawishi na udhibiti wa kigeni katika bara la Afrika. Wareno wakiwa ndio taifa liliofahamika kujihusisha na masuala ya upelelezi pamoja na ngome zao na moto uliodunga msukumo wa kutaka kulijua bara la Afrika kwa undani ili kujua thamani yake, walikuwa wa kwanza kati ya mataifa mengi ya kigeni kutawala pwani ya Afrika Mashariki.
Mombasa na Zanzibar vikawa vitovu vya migogoro na maingiliano ya kitamaduni, kwani Wareno walitimuliwa na Waarabu wa Oman mwishoni mwa karne ya 17, jitihada za biashara za kubadilishana bidhaa na uhusiano wa Waarabu na Oman na wemyeji wa mashariki pwani kuliangazia kuacha mabadiliko ya kudumu katika eneo hilo kupitia kuenea kwa dini ya kiislamu na kuunganishwa kwa mila ya Oman katika utamaduni wa wenyeji. Kufikia mapema karne ya 19, Waomani walikuwa wamehamisha mji mkuu wao kutoka Oman hadi Zanzibar, ambako walitawala eneo la pwani ya Kenya.
Waingereza hatimaye walichukua mamlaka mwishoni mwa karne ya 19 kwa kuanzisha shughuli zao nchini Kenya kama ulinzi na baadaye kama koloni chini yao. Kufurika kwa wafanyabiashara na wahamiaji wa kigeni kutoka Uajemi, India, Uchina, Uhispania, Uturuki, Italia, Ujerumani na Ufaransa kuliboresha zaidi utamaduni wa Afrika Mashariki, huku kila kundi likichangia ukandamizaji wa jamii za wenyeji wa kisiwa Pwani. Lugha ya Kiswahili, ambayo ni mchanganyiko wa lugha za Kibantu, Kiarabu, Kiajemi na baadaye Ulaya, iliibuka kuwa lugha ya kawaida, na kuunganisha jamii mbalimbali za pwani katika utamaduni tofauti za jamii ya Kiswahili.
Kivuli cha biashara ya utumwa (karne ya 16-19)
Kwa kuongezea, enzi hii ya usanisi wa kitamaduni ilitanda giza kwa kukingwa na kivuli cha biashara ya utumwa, janga ambalo lilikumba bara kwa karne nyingi. Zanzibar, hasa chini ya Sultan Sayyid Bargash bin Said al-Busaidi, ikawa kitovu cha biashara hii mbaya, ikihudumia mahitaji ya masoko kutoka Peninsula ya Arabia hadi Amerika. Hatua hii ya kugeuka kwa giza iliambatana na matokeo ya safari za Christopher Columbus, ambazo zilikuwa zimefunua 'Dunia Mpya' kwa matarajio ya Ulaya.
Wenyeji asili wa mkoa huu wa pwani,walijipata katika hali tatanishi walipoanza kuwa watumwa katika ardhi zao, walijikuta wamekamtwa na jinamizi la unyonyaji na upinzani. Wakazi wa eneo hilo walikosa budi ila kukabiliana na hali hii ya unyanyasaji. Upande mwingine wa kisiwa wafanyabiashara wa shughuli za utumwa wa Kiarabu kama bwana Hamad bin Muhammad walipotia nanga katika maeneo kama Zanzibar, wakigeuza wenyeji asili kuwa bidhaa vya kupigwa bei katika masoko ya utumwa.
Zanzibar hasa, iliibuka kama kitovu muhimu katika jitihada izi za biashara ya utumwa, ikikidhi mahitaji ya Peninsula ya Arabia, Iran, Uingereza, na Amerika. Kile kilichoanza kama upeo wa mafanikio kiligeuzwa kuwa jinamizi la tamaa aliyekiuka mipaka, na ufuatiliaji wa utajiri kuzidi thamani ya maisha ya binadamu.
Upinzani na uasi (mapema karne ya 20)
Mwanzoni mwa karne ya 20, upinzani na uasi ulikuwa umekithi umaarufu. MeKatilili wa Menza, mwanamke shujaa na shupavu kutoka jamii ya Giriama, aliibuka kuwa kielezo na kiuongo muhimu katika vita dhidi ya utawala wa kikoloni katika kipindi cha historia ya misukosuko hii ya ukandamizaji.
Uasi wake shujaa huyu haukuwa tu mapambano dhidi ya uvamizi wa Ingereza, bali pia alisisitiza kuwepo kwa msimamo wa utu na uhuru wa wapwani na wa mijijkenda wote na utamaduni wa jamii yake.
Waingereza, wakiongozwa na Malkia Victoria na baadaye Mfalme Edward VII, walilenga kudumisha udhibiti wao kwa kunyonya uchumi wa ndani wa kikoa hiki kwa njia ya udanganyifu wa kibiashara, hasa katika biashara ya meno na pembe za wanyama kama tembo, na kwa kujaribu kuvuruga shuhuli za kilimo kwa wanajamii wa kimijikenda kwa kuwa lazimu kutumia na mazao ya kigeni,pia waliwapokonya mashamba makubwa na sehemu za makao wenyeji ardhi.
Urithi wa ujasiri kwa kupigania uhuru
Ustahimilivu wa jamii ya Wamijikenda ulizidi kusheheni kwa kupinga na kukataa kwao kushindwa na nguvu za ukoloni, na ujasiri uliompa roho ya MeKatilili wa Menza nguvu kila uchao kupinga ukaidi na ukandamizaji unazidi kuonekana na kuwapa wakoloni vizuizi katika hali zao ya shughuli za unyakuzi wa mali na ardhi,walizidi kueneza mikutano ya hadhara hupitia historia za sehemu zengine kama urithi wa nguvu ya kudumu na ustahimilivu kwa watu wanaopigania uhuru na utambulisho wao. Kutoka kujificha na kukabiliana na wakoloni nadani ya msitu ‘Kaya’ takatifu hadi masoko ya Mombasa na vyumba vya mahakama ambapo vita vya haki vilipiganwa, hadithi ya Mijikenda ni moja ya ujasiri, upinzani, na uhusiano usiovunjika mbali kudhihirika kati ya watu na ardhi yao.
Tunaposafiri kupitia kurasa za hadithi hii, tunapitia njia za wakati na mbinu, kutoka siku za kale za ustawi na amani kupitia msukosuko wa uvamizi na upokonyaji kulileta uchungu mno kwa wanajamii asili na kusababisha mvuto na msukumo usiovunjika hadi alfajiri ya enzi mpya iliyotiwa alama na urithi wa wale waliopigana kwa ushupavu,kujitolea na roho isiyoyumba kwa kila kilichowakumba.
Hii sio tu hadithi ya Mekatilili wa Menza au jamii ya wamijikenda. zaidi ni kielezo cha maisha ya wenyeji na wapiganiaji ukombozi katika wimbi la historia, hadithi ambayo inarudia mapambano husika wakati wa uhuru, heshima, na haki ya kuunda hatima ya mtu.